Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amesema sheria mpya ya makosa ya mtandaoni itakula kwa wengi. Msando amesema kuwa utekelezaji wa sheria hiyo si mgumu kama
wengi wanavyodhani na infact wengi wataenda jela. “Ili sheria
itekelezeke huhitaji kushtaki watu wote,” amesema Msando. “
“Huwezi ukakamatwa wewe umemtukana Albert ukasema na Abdalah alimtukana
naye akamatwe. Ukikamatwa wewe tunaanza na wewe. Kwahiyo ukimuona
mwenzio amefungwa miezi sita, miaka saba, miaka mitano, amelipishwa
faini, definitely utaacha.”
“Kwasababu kazi ya sheria ni kwanza kumrekebisha mtu kwa njia ya adhabu
na pili kumsababisha mtu aepuke kufanya jambo kitu fulani. Inapopitishwa
ukiona watu wa kwanza wa pili kweli imetekelezeka, kuna watu wataacha
zile tabia maake watajua sasa hapa ni tatizo. Na umeangalia kabla hata
haijatumika watu wanakuambiwa ‘tutukane ya mwisho mwisho kabla ya hiyo
sheria haijaanza kupitia. Tayari watu wameshajua ni makosa kufanya mbili
tatu.”
Msando amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuheshimiana na kuitumia kwaajili ya maendeleo na kupata taarifa sahihi.
“Mimi nimeitumia vizuri, nimepata wateja zaidi ya watano wa kazi kubwa tu kwa kupitia mitandao ya kijamii.”

No comments:
Post a Comment