Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70
aliyemchoma mkewe mwenye umri wa miaka 16 mjini Mandera kazkazini
mashariki mwa Kenya amekamatwa.
Mke huyo aliyelazimishwa kuingia
katika ndoa mwaka 2014 amelazwa katika hospitali kuu ya Mandera akiwa na
majeraha mabaya ya kifuani pamoja na mikononi, kiongozi mmoja wa
wanawake Ubah Gedi amethibitisha.
Mwanamke huyo sasa tayari amesafirishwa hadi jijini Nairobi kwa matibabu zaidi.
Ufichuaji
huo uliofanywa kuhusu shambulizi hilo ni wa kushangaza kwa kuwa maswala
mengi ya kijinsia Kazkazini mwa Kenya yameendelea bila kuripotiwa.
No comments:
Post a Comment