Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula kuwa Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi
Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.
Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya kuwa naibu Katibu
Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati
Wizarani hapo.
Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015.
| Balozi Liberata Mulamula. |
Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015.
No comments:
Post a Comment