 |
| Ofisa wa polisi akidumisha ulinzi eneo lilipotokea shambulio. |
 |
| Mwanausalama akiwatuliza watu waliohudhuria hafla hiyo baada ya shambulio. |
 |
| Rais wa kundi lililoandaa hafla hiyo la American Freedom Defense Initiative (AFDI), Pamela Geller akiongea na wanahabari. |
 |
| Mfano wa hundi iliyotolewa na kundi hilo kwa mtu atakayechora kibonzo kizuri zaidi cha Mtume Mohammed.. |
 |
| Pamela Geller akiwa kabeba bango katika harakati zake. |
WATU wawili waliokuwa na silaha wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini Texas nchini Marekani.
Watu hao waliwashambulia walinda usalama kwa risasi katika eneo la
hafla moja yenye utata ya uchoraji wa vibonzo vya kuwakejeli Waislamu na
Mtume Mohammed jana.
Shambulio hilo lilifanyika mjini Dallas mahali ambapo kulikuwa na onyesho hilo.
Hafla hiyo iliandaliwa na Kundi la American Freedom Defense
Initiative (AFDI), linaloongozwa na Rais wao, Pamela Geller ambalo
limekuwa likikejeli Uislamu.
Kundi hilo lililokuwa litoe zawadi nono ya dola milioni 12.5 kwa
mchoraji kibonzo kizuri zaidi atakayeibuka mshindi kwa kumchora Mtume
Mohammed.
No comments:
Post a Comment