Nepal imewataka watoa huduma za
misaada ya kigeni kwenye mji mkuu Kathmandu na maeneo yanayozunguka mji
huo kurudi makwao ikisema kuwa asiliamia kubwa ya kazi imekamilika.
Serikali inasema kuwa oparesheni za uokoaji zilizosalia maeneo ya mbali ya vijijini zinaweza kufanywa na polisi na jeshi.
Tangu nchi hiyo ikumbwe na tetemeko la ardhi siku 9 zilizopita zaidi ya watoa huduma 4000 kote duniani wamekuwa wakisadia kutoa misaada na oparesheni za ukoaji.
No comments:
Post a Comment