 |
| Rapa Rick Ross ‘Ricky Rozay’. |
MPIGA picha
maarufu nchini Marekani, Armen Djerrahian, anaweza kujikuta katika vita
ya maneno na rapa Rick Ross ‘Ricky Rozay’ baada ya kumpiga mkwara rapa
huyo juu ya matumizi ya picha za Jay Z.Ross na Jay Z wamekuwa ni
marafiki wa muda mrefu huku wakishirikiana kufanya kazi kadhaa pamoja.
 |
| Mpiga picha maarufu nchini Marekani, Armen Djerrahian. |
Lakini Djerrahian ambaye ni mpiga picha wa Jay Z, amemshupalia Ross
na kumueleza kuwa hata kama yeye ni rafiki wa rapa huyo mmiliki wa lebo
ya Roca Fella lakini haruhusiwi kutumia picha zake bila
idhini.Djerrahian, alifikia hatua hiyo baada ya Ross kutupia picha ya
Jay Z ambayo ilipigwa 2003 kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.
Djerrahian alifika mbali baada ya kumlaumu Ricky Rozay ambaye
aliitumia picha hiyo kwenye video ya wimbo mpya wa "Movin Bass" ambao
amemshirikisha Jay Z.
No comments:
Post a Comment