Fiji ilipewa taji hilo kufuatia ushindi wake dhidi ya Afrika Kusini kwenye robo fainali iliyochezwa Twickenham. Savenaca Rawaca alifunga ''try'' mbili huku nahodha Osea Kolinisau akivuka mstari wa choka wa Afrika Kusini na kuipa Fiji taji lao la pili tangu mwaka wa 2006.
Ufanisi wa Fiji umeifanya kuwa nchi ya pili baada ya New Zealand kushinda kombe la Sevens series tangu 2010. "Ahsanteni sana kwa kuishabikia hii timu,".
Kolinisau aliiambia tovuti ya Raga duniani. ”Kuwa kikosi cha pili cha Fiji kushinda taji hili ni hisia kubwa”.
"Tunashukuru sana tumemaliza msururu huu, imekuwa ni safari ndefu,.
Timu za Fiji, Afrika kusini, New Zealand, na Uingereza, zimefuzu kwa mashindano ya raga ya Olimpiki kwa wachezaji saba yatakayofanyika Rio, Brazil
baada ya kuchukua nafasi nne za kwanza katika msururu wa raga duniani mwaka huu.
Mwenyeji Brazil atakamilisha oradha ya timu za raga zitakazoshiriki kwenye Olimpiki.
No comments:
Post a Comment