Mamilioni ya watu watakuwa wakipiga kura katika uchaguzi mkuu wa Uingereza leo Alhamisi
Vituo vya kupigia kura karibu 50,000 nchini kote vitafunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za Uingereza.Kama ilivyo kwa uchaguzi mkuu, kuna viti zaidi ya 9,000 vya madiwani vinavyogombewa katika serikali za mitaa 279. Mameya pia watachaguliwa katika miji ya Bedford, Copeland, Leicester, Mansfield, Middlesbrough na Torbay.
Masanduku ya kupigia kura yamepelekwa katika vituo vya uchaguzi.
Kwa mara ya kwanza, watu waliweza kujiandikisha kupiga kura kupitia njia ya mtandao.
Vituo vingi vya kupigia kura viko katika majengo ya shule, kumbi za vituo vya kijamii na kwenye kumbi za parokia, lakini migahawa, maeneo ya kufua na kunyosha nguo na basi la shule pia vitatumika kama vituo vya kupigia kura.
Vituo vya kupigia kura vitafungwa saa nne usiku kwa saa za Uingereza, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema mtu yeyote ambaye atakuwa kwenye mstari kufikia wakati huo ataweza kupiga kura yake.
BBC itatangaza moja kwa moja kuanzia saa tatu na dakika 55 usiku shughuli za uchaguzi katika kaunti 220.
Matangazo kamili kuhusu matokeo yanavyopokelewa yatakuwa katika ukurasa wa mtandao wa BBC politics online live na katika sehemu ya mbele ya ukurasa wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na taarifa zote mpya kutoka sehemu mbalimbali nchini na uchambuzi wa waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment