Kila
mwanamichezo au mwanamuziki hulipwa mshahara kulingana na kiwango
chake, hali hii ipo hivyo pia kwa waigizaji na watu wengine wa kawaida.
Hali
hii imekuwa ikiwapa morali zaidi wale wanaofanya kazi kujituma ili
wapate mshahara mkubwa zaidi au kupewa kazi ya ziada tofauti na pale
ulipozoea.
Hii
pia imekuwa ikifanyika kwa wasanii wa filamu za Tanzania wenye umoja
wao maarufu kama Bongo Movies. Hao wamekuwa wakilipwa madau kama
wachezaji ili wafanye kazi za wenzao, hii imekuwa ikileta changamoto
kubwa kwa wasanii kuhakikisha wanapanda dau kutokana na uwezo binafsi.
Asilimia
kubwa ya mashabiki wa filamu za kibongo wamekuwa wakitoa fedha za
kununua kazi zao bila kufahamu muhusika ‘anayemnunua’ amelipwa kiasi
gani cha fedha kucheza ‘movie’ aliyoinunua. Tazama bei zao hapa chini:
Vincet Kigosi ‘Ray’
Inadaiwa
kuwa huyu jamaa ni mgumu sana kukubali kucheza filamu za watu.
Alishawahi kupewa Sh Milioni 10 ili cheze filamu moja (jina kapuni)
lakini aligoma na amekuwa na msimamo mkubwa katika kazi zake lakini
badala yake hizo fedha zikawalipa wasanii wengine watatu.
Inaaminika
ndiye msanii mwenye gharama kubwa licha ya kuwa mpaka sasa bado amekuwa
akigoma kucheza filamu za wenzake, ishu kubwa akidaiwa kujiona ni
‘staa’ zaidi ya wenzake.
Wema Sepetu
Kipaji
chake kiliibuliwa na marehemu Steven Kanumba kupitia Filamu ya ‘A Point
Of No Return’ baada ya hapo akapata mashavu kibao na hadi sasa
amefanikiwa kucheza filamu na msanii mkubwa Van Vicker raia wa Ghana.
Wema Sepetu
Za
mjini zinasema kabla hajaachana na aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake,
Clement alikuwa akitoza kuanzia Sh Milioni Tano kwa filamu moja lakini
sasa anapokea hata chini ya hapo kwa kuwa fedha zimeanza ‘kumkatikia’.
Wema
ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2006, alizaliwa mwaka 1988, Dar
anamiliki kampuni yake inayofahamika kama Endless Fame Films na ndiye
mkurugenzi mtendaji.
Kajala Masanja
Ana
kampuni yake ya uzalishaji wa filamu inayoitwa Kay Entertainment na
tayari ameshafanya kazi zake zinayofahamika kwa majina ya Mbwa Mwitu
pamoja na Pishu.
Lakini
linapokuja suala la kufanya kazi za watu inakulazimu kuzama katika
pochi au ‘waleti’ ukitoa mkono uwe na Sh Milioni Mbili lakini kwa kiasi
hiki awe anakufahamu na kama ‘ndo’ mnaona kwa mara ya kwanza jiandae
kuachia Sh Milioni Tatu hadi 2.5 zaidi ya hapo hakuna maneno maneno kazi
inapigwa kwa kiwango kikubwa tu na binti huyu aliyezaliwa mwaka 1983.
Jacqueline Walper ‘Wolper’
Ninja,
dada mkubwa, anaweza kucheza ‘sini’ zote ziwe za kijambazi, mke mwema
na hata changudoa, amekuwa na mashabiki wengi sana Bongo na hata nje
ambao wamekuwa wakipenda kazi zake.
Mshkaji
huyu ambaye alizaliwa mwaka 1987 huko Moshi, Kilimanjaro, yupo kishkaji
tu kwani anakubali kupokea kuanzia Sh Milioni 2 hadi 2.5 hapo haipungui
labda iongezeke ndipo atakufanyia kazi zako. Mpaka sasa amecheza filamu
zaidi ya 20.
Mzee Majuto
Licha
ya kuzaliwa mwaka 1948 huko Tanga, Amri Athuman ‘King Majuto’ au Mzee
Majuto bado inaaminika kuwa ndiye msanii mwenye mashabiki wengi zaidi
Bongo kutokana na uimara wa kuigiza hususan kwenye filamu za kuchekesha.
Mzee
wa watu hana makuu ukitaka achekeshe weee filamu nzima jiandae kumkatia
Sh Milioni 1.5 hadi 2 tu, hicho ndicho kiwango chake na atakufanyia
kazi kwa umakini mkubwa zaidi ya hapo hashuki. Nje ya fani anamiliki
daladala mbalimbali huko kwao Tanga ambazo pia zinamuongezea kipato.
Riyama Ally
Anaigiza
kwa hisia kali sana katika kila filamu, ukitaka alie na machozi yatoke
kwa wingi au acheze filamu za kimbea, majungu, vigodoro na nyinginezo
wala hana makuu dada wa watu anapokea hata Sh Milioni 1.5.
Riyama
ambaye alianza kujihusisha na maigizo mwaka 2000 akiwa na kundi la
Taswira, mara nyingi katika filamu alizocheza anasifika kwa kuigiza kwa
uhalisia mkubwa pengine ukimtoa Johari wa enzi za Tamthilia ya Johari
basi huyu ni namba mbili kwa wepesi wa kutoa machozi. Mpaka sasa
amecheza filamu zaidi ya 40.
Blandina Chagula ‘Johari’
Alipata
jina kupitia Tamthilia ya Johari kabla ya kuhamia kwenye filamu. Ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya RJ akisaidiana na msanii mwenzake Ray, katika
kuindesha. Diva huyu wa movie za Kibongo alizaliwa mwaka 1983 huko
Shinyanga.
Hana
makuu katika kusaidia wenzake na mara nyingi amekuwa akijitoa kwa moyo
kucheza filamu yoyote. Dau lake ni la ki-upendo zaidi kwani anapokea
hata Sh Milioni Moja, hii yote anafanya kwa lengo la kusaidia wenzake.
Anasifika
zaidi kwa kucheza filamu za kulialia kwani kwake kutoa machozi si
lolote hata sekunde mbili hazipiti anakuwa kayatiririsha hatari.

No comments:
Post a Comment