Mfanyikazi mwengine wa hospitali hiyo alisema kuwa wafanyikazi wenzake walishikwa na hofu na wakakimbilia usalama wao. Wanajeshi wanne waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo walichukuliwa na hadi sasa hatma yao haijulikani.
Mapema ijumaa watu 18 wanaoshukiwa kupanga ''mapinduzi'' hayo, walifikishwa mahakamani lakini kiongozi wao mkuu meja jenerali Godefroid Niyombare hajulikani aliko. Hapo jana rais Nkurunziza aliwapongeza wanajeshi waaminifu kwa uadilifu wao na ukakamavu uliowawezesha kudhibiti ''wasaliti'' waliokuwa wametangaza ''Mapinduzi'' na kutaka kutibua vita na umwagikaji wa damu nchini humo.
Bwana Miburo alisema kuwa walikuwa wamepigwa sana hasa Jenerali Ndayirukiye.amaa zao walisema kuwa walikuwa wamepigwa sana na hata kupoteza uwezo wa kusikia kutokana na kipigo.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Karen Allen amesema kuwa maafisa wa jeshi wanne waliburutwa kutoka hospitalini walipokuwa wakipokea matibabu mmoja wao aliaga dunia.
Hali ya usalama ilizorota nchini Burundi kuanzia tarehe 26 Aprili, rais Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania awamu ya tatu katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi juni.
Wapinzani wake wanadai kuwa Nkurunzinza anakiuka mwafaka wa amani uliowekwa unaomruhusu rais kutawala kwa vipindi viwili pekee.
Watu 25 wamethibitishwa kufariki huku zaidi ya laki moja wakitorokea mataifa jirani wakihofu kutibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment