Pages

Wednesday, 27 May 2015

Wafahamu washukiwa wa vitendo vya rushwa

FIFA, shirikisho lenye utajiri wa mabilioni ya dola za Kimarekani ambalo linasimamia mchezo wa soka duniani,limekumbwa na kashfa ya rushwa kwa miongo mingi, ambapo maafisa wa ngazi ya juu wa soka walikamatwa mapema Jumatano.
Rais wa CONCACAF
 Huku viongozi wa FIFA wakikutana mjini Zurich, Jumatano, maafisa wa polisi waliwasili katika hoteli moja ya nyota tano ya Baur au Lac kuwakamata baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo la soka duniani kwa ombi la wizara ya sheria ya Marekani.

Bwana Blazer alikiri kosa mwaka 2013 kwa makosa 10, iikiwa ni pamoja na ulaghai, udanganyifu wa fedha kupitia mtandao na njama za kutenda makosa na kulipa faini ya dola milioni 1.9za Kimarekani. Watu wengine watatu - wakiwemo watoto wawili wa kiume wa afisa wa soka kutoka eneo la Caribbean Jack Warner - pia kampuni mbili za masoko za masuala ya michezo pia zilikiri makosa.
• Katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Zurich, msemaji wa FIFA amesema hali ilikuwa nzuri kwa shirikisho lake kwa sababu ilionyesha kuwa FIFA ina shauku ya kubadilika. Pia amesema shirikisho hilo haitafungua mchakato wa maombi ya kuandaa fainali za mwaka 2018 na 2022, japokuwa maafisa wa Uswisi wamesema wafungua uchunguzi sambamba na kukamata nyaraka na data za kielektroniki kuhusiana na masuala hayo.
• Mwanasheria Mkuu wa Marekani Loretta E. Lynch, ambaye aliingia madarakani mwezi uli na Mkurugenzi wa F.B.I. James Comey wanatarajiwa kuitisha mkutano wa waandishi wa habari Jumatano saa 04:30 asubuhi mjini Brooklyn.
Nani wanashitakiwa?
Jeffrey Webb: Rais wa shirikisho la soka kwa vyama vya Amerika ya Kati Concacaf, moja ya mashirikisho sita ya kimaeneo yanayounda shirikisho la FIFA, na makamu rais wa FIFA.

No comments:

Post a Comment