Jaji wa Mahakama ya Afghan
amewahukumu wanaume wanne adhabu ya kifo kwa muua kwa kumshambulia
mwanamke mmoja mjini Kabul zaidi mwezi mmoja uliopita.
Waandamanaji wakipinga mauaji ya Farkhunda
Mwanamke
huyo anayeitwa Farkhunda alipigwa hadi kufa na kundi la watu wenye
hasira baada ya kutuhumiwa kimakosa kuchoma kitabu cha Koran.
Mwili
wake ulichomwa mwoto. Watu wengine 49 wanaendelea na kesi, wakiwemo
polisi 19 wanaotuhumiwa kwa kushindwa kuingilia kati kumwokoa mwanamke
huyo.
Mauaji hayo yalisababisha hasira kutoka maeneo mbali mbali
duniani ambayo pia yalisababisha maandamano nchini Afghanistan kupinga
jinsi mwanamke huyo alivyotendewa.
No comments:
Post a Comment