Mwenyekiti Kamati ya maandalizi ambaye pia ni
Katibu Mkuu wa Yanga Tawi la Tabata Kisiwani, Brito Burure, aliliambia
Mwanaspoti akisema: “Mipango yote kwa ajili ya kufanisha shughuli hiyo,
imefikia pazuri.
“Lengo ni kuwakutanisha Wanayanga nchi nzima na kusheherekea mafanikio ya klabu yao kwa pamoja.
“Lakini tunataka kuwapongeza wachezaji wetu kwa
kuwapa tuzo kwa kazi nzuri waliyofanya hadi kuwa mabingwa na watatakiwa
kufika kufurahia ushindi huo pamoja na familia za.”
Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kutunukiwa
tuzo hizo ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu, Simon Msuva, pamoja na viongozi
na makocha waliofanikisha Yanga kutisha katika msimu huo ulioisha.
Kuhusu kitabu hicho alisema kimebeba simulizi ya historia nzima ya klabu hiyo.
Kwa upande wa mwandishi wa kitabu hicho cha Yanga,
Ching’ole alisema: “Nimeamua kuandika kitabu hicho, ili Wanayanga
waitambue klabu yao kwa undani zaidi.”
No comments:
Post a Comment