Ajuza aokolewa katika boti iliozama China
Waokozi nchini Uchina wanaowasaka
manusura kutoka kwenye meli ya abiria iliyozama katika mto Yangtze
wameweza kumvuta kutoka kwenye meli hiyo mwanamke mwenye umri wa miaka
85.
Mwanamke huyo ni mmoja wa watu wapatao 12 wanaofahamika
kunusurika katika ajali hiyo iliyotokea baada ya meli hiyo kuzama jana
usiku.
Miili ya watu imekuwa ikivutwa kutoka kwenye meli hiyo. Watu zaidi ya 450 walikuwa wameabiri meli hiyo ilipopata ajali kutokana na hali mbaya ya hewa.
No comments:
Post a Comment