 |
| Mpiganaji wa Al Shabaab, Thomas Evans aliyeuawa kwenye mapigano ya kundi hilo dhidi ya Jeshi la Kenya, anadaiwa kuwa raia wa Uingereza . |
 |
| Wapiganaji 11 wa Al Shabaab waliouawa baada ya mapigano makali na Jeshi la Kenya huko Lamu, Kenya. |
 |
| Evans katika muonekano wa Al Shabaab. |
 |
| Evans alisafiri kutoka nyumbani kwao High Wycombe, Buckinghamshire nchini Uingereza mpaka makao Makao Makuu ya Al Shabaab. |
 |
| Wanajeshi wa Kenya wakiwa katika harakati za kupambana na kundi la Al Shabaab. |
MWINGEREZA aliyebadili dini na kuwa Muislam, Thomas Evans, 25,
ameuawa mwishoni mwa wiki akiwa anapigana na kundi la Al-Shaabab wakati
likiendesha mapigano nchini Kenya.
Inaaminika mtu huyo kutoka High Wycombe, Buckinghamshire, Uingereza,
alikuwa mmoja wa wapiganaji 11 waliouawa wakati waliposhambulia kituo
kimoja cha jeshi kaskazini mwa Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Evans, alisilimu na kubadili jina lake na kuitwa Abdul Hakim na mnamo
mwaka 2011, akiwa na umri wa miaka 19, Evans alijiunga na kundi hilo
ambalo limesema lilifanya shambulio hilo Wilaya ya Lamu na “kuua askari
wengi wa Kenya” lakini bila kutaja idadi ya wapiganaji wake waliouawa.
Wataalam wa serikali wanachunguza vinasaba vya mtu huyo kuhakikisha
kama kweli ni yeye. Pia kuna mtu mwenye asili ya Kiarabu ambaye ni
miongoni mwa waliokufa, mbali na wengine ambao wanaonekana ni wenye
asili ya sehemu waliyouawa.
No comments:
Post a Comment