Jeshi nchini Korea Kusini linasema
kuwa mwanajeshi wa Korea Kaskazini ametoroka nchi hiyo na kuingia nchini
Korea Kusini akipitia mpaka wa mkoa wa Gangwo, Mwanajeshi huyo mwenye umri wa makamo alivuka mpaka huo kwa miguu.
Kuhama kwa wanajeshi kupitia mpaka huo ulio chini ya ulinzi mkali si jambo la kawaida.
Korea
Kusini ilichukua hatua za kuboresha ulinzi kwenye mpaka kufuatia tukio
la mwaka 2012 wakati mwanajeshi mwingine kutoka Korea Kaskazini alivuka
mpaka usiku wa manane na kuingia nchini Korea Kusini.
No comments:
Post a Comment