Bosi huyo alisema beki huyo raia wa Nigeria atakuja nchini wakati wowote kuanzia wiki ijayo kuja kukamilisha usajili wake huo, huku pia wakiendelea kusaka saini ya mshambuliaji Mohamed Traore anayekipiga El Merreikh ya Sudan.
Usajili wa Traore ambaye ameonekana kuwavutia
zaidi mabosi wa juu wa klabu hiyo, utakamilika tu endapo El Merreikh
watapata mbadala wake ambapo klabu hiyo imemwambia itamuachia kama hilo
litakamilika.
“Tunamleta huyo beki ingawa kwa sasa hatuwezi
kukutajia jina, lakini ni raia wa Nigeria alikuwa anacheza soka Ulaya
atakuja kuchukua nafasi ya Mwantika,” alisema bosi huyo. Mwantika
anatajwa kutaka kutua Simba baada ya kumaliza mkataba wake na
Wanalambalamba hao.
No comments:
Post a Comment