Pages

Wednesday, 3 June 2015

Mbeya City mambo ni kimyakimya

KLABU ya Mbeya City imeamua kufanya usajili wake kim ya kimya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kuzingatia mapendekezo ya kocha, Juma Mwambusi. Haitaki kuwa kama Simba na Yanga zinazosajili kwa mbwembwe.

Tayari Mbeya City imeshawasainisha wachezaji wawili wapya akiwamo beki Haruna Shamte wa JKT Ruvu na mshambuliaji wa Coastal Union, Joseph Mahundi. Hata hivyo usajili wa wachezaji hao umefanywa kwa kushtukiza na msemaji wa timu hiyo, Dismas Teni alilidokeza gazeti hili kuwa wameshapokea mapendekezo ya kocha Mwambusi, lakini wanafanya kazi zao kimya kimya bila makeke ili kuijenga timu imara kwa msimu ujao.
“Nimepigwa stop kuzungumzia usajili, lakini tunaendelea na yetu kwa ajili ya kuijenga timu kabambe ya msimu ujao kwa kuzingatia kile ambacho benchi la ufundi limeagiza kifanywe,” alisema.
Kuhusu kuondoka kwa nyota wao, Deus Kaseke na Peter Mwalyanzi waliojiunga na Yanga na Simba, Teni alisema mashabiki hawana sababu ya kuwa na hofu kwani Mbeya City ina hazina kubwa ya wachezaji ambao wataifanya timu hiyo kuzidi kukimbiza Tanzania.
Alikiri Kaseke na Mwalyanzi waligoma kusainia mikataba mipya na wao hawakuwa na jinsi kwani tayari walishajua wapi wanapoenda kwani walishatakiwa tangu ulipoisha msimu wao wa kwanza katika Ligi Kuu walipomaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga.

No comments:

Post a Comment