MSHAMBULIAJI wa kimataifa Zimbabwe anayeichezea FC Platnum ya
kwao, Donald Ngoma, anayehusishwa na mipango ya kutua Jangwani,
amefungua kinywa chake na kutamka maneno machache tu akisema: “Yanga ni
watamu sana. ”Ngoma ambaye anahitajiwa na kocha wa Yanga,
Mholanzi Hans Pluijm, ambaye alithubutu kusema Didier Kavumbagu wa nini
wakati unaweza kuwa na mtu kama huyu (Ngoma).
Donald Ngoma, Mshambuliaji wa PLatnum Fc ya Zimbabwe
|
Kufuatia taarifa nyingi Mwanaspoti liliamua
kumsaka mshambuliaji huyo na kufanya mazungumzo naye kwa njia ya simu ya
mkononi na akaeleza kila kitu kuhusu kinachomchelewesha kutua kwake kwa
Mabingwa hao wa Tanzania;
Mwanaspoti: Habari yako Donald Ngoma
Ngoma: Salama. Nazungumza na nani?
Mwanaspoti: Unaongea na mwandishi wa gazeti bora la michezo Tanzania la Mwanaspoti.
Ngoma: Nashukuru, niambie.
Mwanaspoti: Vipi maendeleo yako na hapo ulipo FC Platinum?
Ngoma:Kila kitu kinaendelea vyema tunaendelea na ligi, japo leo (jana Jumapili) tupo mapumziko kidogo.
Mwanaspoti: Ngoma, hapa Tanzania kuna taarifa nyingi juu yako kuhusu kuja huku likoje hili?
Ngoma: Kuna uwezekano wa hilo kama kila kitu kitakwenda sawa.
No comments:
Post a Comment