Aliyekuwa kocha wa Napoli Rafa Benitez amethibitishwa kuwa k ocha wa Real Madrid katika kandarasi ya miaka mitatu. Benitez
mwenye umri wa miaka 55 anachukua mahala pake Carlo Ancelotti ambaye
aliondoka katika kilabu hiyo miezi 12 tu baada ya kuisaidia kushinda
kombe lao la kumi la vilabu bingwa Ulaya.
 |
| Rafa Benitez |
Benitez ambaye ni
mzaliwa wa Madrid amehudumu misimu miwili kama mkufunzi wa Napoli ,baada
kufanikiwa na vilabu kadhaa vya Ulaya.
Baada ya kuisaidia
Valencia kushinda kombe la Uefa mwaka 2004,mwaka unaofuatia alielekea
Liverpool na kuisaidia kilabu hiyo kushinda kombe la vilabu bingwa ikiwa
ni msimu wake wa kwanza katika kilabu hiyo ya Mersyside.
Miaka
miwili baadaye aliisaidia Liverpool kufika katika fainali za kombe la
vilabu bingwa Ulaya na mwaka 2013 alikuwa kaimu mkufunzi wa Chelsea
waliposhinda kombe la Yuropa.
No comments:
Post a Comment