NAHODHA wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amefurahishwa
na ujio wa jezi mpya za timu hiyo akitamba kuwa zitawahamasisha kufanya
vizuri. Cannavaro alitoa kauli hiyo jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa
jezi mpya za timu ya Taifa ulioenda sambamba na ugawaji vyeti kwa
makundi mbalimbali yaliyotoa mchango kwenye maendeleo ya soka hapa
nchini.
“Hizi jezi mpya ni nzuri na zinatia hamasa hasa kutokana na kuwa na rangi zote za bendera ya Taifa jambo ambalo linatupa deni kubwa sisi wachezaji kuipigania timu yetu ya Taifa.Sisi kama wachezaji tunaahidi kupambana ili kutowaangusha Watanzania,” alisema Cannavaro.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
jezi ambazo zitatumika kwa ajili ya mechi za ugenini zitakuwa za rangi
nyeupe wakati zile za rangi ya bluu zitatumika kwa ajili ya mechi za
nyumbani.
Wakati huohuo kikosi cha Stars kinaondoka leo
Alhamisi kwenda Ethiopia kuweka kambi ya siku saba kabla ya kuivaa Misri
kwenye mechi ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika
(Afcon).
No comments:
Post a Comment