| Staa wa muziki wa RnB, Chris Brown. |
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwenye mitandao mbalimbali ya burudani, Chris alianza kumfuatilia ex wake huyo usiku kwenye Klabu ya Playboy huko Chicago ambapo alichukua siti ya VIP iliyo jirani na Karrueche ili iwe rahisi kuonana naye.
| Karrueche Tran akiondoka kutoka katika Klabu ya Playboy huko Chicago, Marekani. |
Mara baada ya Karrueche kuingia kwenye gari yake, Chris alijaribu kutaka kumfuata lakini alizuiwa na marafiki wa modo huyo, ndipo baba Royalty akaamua kulifuata gari lake na kuanza kumfuata kwa nyuma hadi nyumbani.Alipofika akakuta mlango umefungwa ndipo akaanza kupiga kelele sambamba na rafiki zake aliokuwa nao akitaka afunguliwe, hapo tayari ilikuwa usiku mkubwa.
Kuona hivyo Karrueche aliamua kuondoka na kwenda mgahawani ili kuondokana na kero ya kelele lakini Chris alimfuata na huko kabla ya kusikika majibizano baina yao, muda kidogo modo huyo akaonekana akiondoka eneo hilo akiwa peke yake na kuelekea nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment