| Hawa ni miongoni mwa Watanzania waliohamasika kutembelea katika viwanja vilivyokuwa kwenye mradi wa Vikuruti kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambavyo vinatolewa kwa wananchi kwa mkopo. Wakopaji ni watumishi wa umma, kampuni binafsi na wajasiriamali. |
| Eneo la viwanja vya Vikuruti vinavyoonekana huku barabara ikionekana pichani. |
WATANZANIA
wameendelea kuvichangamkia viwanja vya mkopo vinavyotolewa na Taasisi
ya Kifedha ya Bayport Financial Services, vilivyopo Vikuruti, wilayani
Kibaha, mkoani Pwani.
Kuchangamkiwa kwa
viwanja hivyo kumekuja siku chache baada ya kuzindua huduma mpya ya
mikopo ya viwanja hivyo kutoka Bayport, ikiwa ni ishara nzuri na njia ya
kuwapa fursa Watanzania ya kumiliki nyumba.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo,
alisema watu wengi wamekuwa wakituma maombi ya kuomba kupewa viwanja
hivyo, tangu huduma hiyo ilipozinduliwa rasmi.
Alisema kwamba baadhi ya watu walioonyesha
nia ya kuvipata viwanja hivyo pamoja na kutuma maombi yao, pia wamekuwa
wakitembelea eneo kulipokuwa na viwanja hivyo ili wajiridhishe kwa ajili
ya kujipatia viwanja hivyo vinavyokopeshwa kwa minajiri ya kuwakwamua
Watanzania, ukizingatia kuwa ardhi inapanda thamani siku hadi siku.
“Jana (juzi) zaidi ya watu 82 wamekwenda
Vikuruti, Kibaha kujionea eneo lenyewe na kuchagua viwanja wapendavyo,
ikiwa ni mwendelezo mkubwa wa wananchi wanaotuma maombi ya kukopa
viwanja vya Bayport, wakichukua fomu bure z kwa kupitia matawi yetu
yaliyoenea nchi nzima, bila kusahau kwenye matawi ya Bank of Afrika
(BOA).
“Huduma hii ni murua kwa Watanzania wote,
tukiamini kuwa ni sehemu ya kuwapatia wananchi urahisi wa kumiliki vitu
vyenye thamani ikiwamo ardhi wanayoweza kuitumia kwa mambo mengi, ikiwa
nyumba za kuishi na za biashara, huku thamani ya viwanja vikianzia Sh
1,400,000 na kuendelea kwa viwanja vyenye ukubwa tofauti vya kujenga
nyumba za kuishi na biashara kama vile shule, vituo vya afya, nyumba za
kulala wageni na hoteli,” alisema Cheyo.
Cheyo alisema nafasi ni chache, maana
maombi yanafanyika kwa siku (20), kuanzia Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu
za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial
Services na matawi ya bank of Africa (BOA), ambapo malipo ya awali
yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport
iliyopo BOA.
Kwa mujibu wa Cheyo, fomu ya maombi na
nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za
taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima na baada ya Juni 10, mteja
atatakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka kwenye
taasisi yao huku watumishi wa umma na wa kampuni binafsi wakiweza
kukopeshwa kiwanja na kukabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90)
watakapokamilisha mkopo wao.
No comments:
Post a Comment