| Jopo la Majaji, Kutoka Kulia ni Zephaniah Muggitu wa Digital Consulting Ltd, Jairos Mahenge Mhifadhi Mwandamizi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development. |
| Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi Oxfam akikaribisha majaji kwa ajili ya kutaja majina ya washindi watakao ingia shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015. |
| Mmoja wa majaji, Zephaniah Muggitu akieleza kwa ujumla namna ambavyo mchakato wa kuwapata washindi hao ulivyokuw. |
Bi. Dora Myinga ambaye pia
alikuwa Jaji akisoma majina ya washindi 18 walioingia katika Shindano la
Mama Shujaa wa Chakula 2015.
|
| Mmoja wa Majaji, Roselyn Kaihula akielezea namna ambavyo fomu zilichambuliwa na kupatikana washindi 18. |
Bi. Mwandiwe Makame akishukuru juhudi za serikali katika kuendeleza na kukuza kilim.
|
| Bw. Jairos Mahenge ambaye akizungumzia kwa ufupi changamoto walizokutana nazo wakati wa mchakato mzima wa kuhakiki fomu za kuwapata washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula. |
| Ofisa Mahusiano ya Ushawishi wa Oxfam Tanzania, Suhaila Thawer akitoa maelezo mafupi ya Jinsi watakavyowatembelea washindi 18 katika maeneo walipo ili kuona shughuri zao na baadae kuwapata washiriki 15 ambao ndio wataingia katika mshike mshike wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015 |
*********
Baada ya zoezi la kupokea na kusahihisha
fomu za washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 kukamilika,
takribani washiriki 18 kutoka mikoa tofauti nchini wamefanikiwa kupita
katika mchujo wa kwanza kabla ya washiriki watatu kuyaaga mashindano
hayo na kubakia 15 ambao ndiyo wataingia kijijini kwa ajili ya kumpata
mshindi.
akizungumza na waandishi wa habari mmoja
wa majaji waliohusika katika zoezi la kusahihisha fomu za washiriki,
Zephania Mugittu alisema kuwa idadi ya washiriki waliowasilisha fomu zao
ni 26,500 ambapo fomu zilizokidhi viwango zikiwa 2,317 tu.
Jaji huyo aliongeza kuwa fomu za
washiriki 21 ndiyo zilizovuka alama zaidi ya asilimia hamsini huku
vigezo vya umri, shughuli za kilimo cha mazao ya chakula, uvuvi na
ufugaji vikiwabakiza washiriki 18 wenye alama za juu kutoka mikoa
tofautitofauti.
Naye Ofisa Mahusiano ya Ushawishi wa
Oxfam Tanzania Suhaila Thawer alimalizia kwa kusema washiriki 18 wote
watatembelewa maeneo waliyopo kuhakikisha kama wanafanya kazi hizo kweli
na baadae kuanza rasmi mchakato wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015.
Washiriki hao 18 ni Getrude Bundala
Deonatus(35) Ukerewe Mwanza, Winnie L. Mallya (24) Kilimanjaro Moshi,
Dina Samwel Sumari (62) Meru Arusha, Tatu Ramadhani Kilua (48) Lushoto
Tanga, Edna Gabriel Kiogwe (40) Ilala Dar es salaam, Neema Hilonga (35)
Hanang Manyara, Pili Kashinje Itamba (30) Kaskazini(U), Eva Mageni
Daudi (31) Bagamoyo Pwani, Hawa Athumani Mkata (56) Masasi Mtwara,
Wandutha Daud Kitoelth (48) Mkalama Singida, Shida Daudi Mwedugo (35)
Chamwino Dodoma, Hellen Materu (36) Iringa Mjini, Upendo Paulo Mhomisoli
(35) Njombe, Savera Xeveri Mutahyabarwa (65) Bukoba Mjini Kagera,
Carolina Humphrey Chelele (48) Kilombero Morogoro, Stella Fabian
Masulya (42) Ukerewe Mwanza, Regina Kapili Stephano (19) Mpanda
Katavi, Rehema Daniel Lukali (46) Sumbawanga Rukwa.
WEKEZA KWA WAKULIMA WANAWAKE WADOGO WADOGO INALIPA
No comments:
Post a Comment