Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini
Oscar Pistorius aliyepatikana na hatia ya mauaji ya mpenzi wake Reeva
Steenkamp huenda akaachiliwa huru tarehe 21 Agosti. Kwa mujibu wa
taarifa za idara ya magereza ya Afrika Kusini mwanariadha huyo
aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huenda akasamehewa.
Mwanariadha mlemavu kutoka Afrika Kusini Oscar Pistorius huenda akaachiliwa huru Agosti tarehe 21
Pistorius alikuwa amefungwa mwaka uliopita kati kesi iliyovutia hisia kali kutoka kote duniani.
Pistorius alimpiga risasi mpenziwe ''akidhaniwa kuwa ni mwizi'' usiku wa siku ya wapendanao. Kiongozi wa Mashtaka Gerrie Nel alidai kuwa Pistorius alimpiga risasi na kumuua bi Steenkamp baada ya wawili hao kuzozana.
Kiongozi wa Mashtaka Gerrie Nel ameomba mahakama imuongezee adhabu
Kiongozi wa Mashtaka amekata rufaa ya kuachiliwa kwake na mahakama
kuu ya rufaa imeratibiwa kuanza kusikiza kesi hiyo mwezi Novemba.
Bwana
Nel anaitaka mahakama hii kumuongezea Pistorius kifungo ijapokuwa mmoja
wa jamaa zake Pistorius amedai kuwa mwanariadha huyo atasamehewa kabla
ya mwisho wa Agosti mwaka huu.
No comments:
Post a Comment