Inakisiwa kuwa mpaka kufikia mwa 2017, zaidi ya Waafrika million mia sita watafaidika na mpango huu. meetingMkutano wa maafisa wa biashara nchini Misri unaendelea huku wakiwa katika hali ya mashaka kukamilisha mpango huo.
Inaarifiwa kuwa mpango huo utakuwa tayari kusainiwa hii leo.
Baada ya hapo, mapatano hayo yatazinduliwa rasmi kwenye mkutano wa umoja wa Afrika mwishon mwa juma hili. Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, jumuia ya kibiashara ya Afrika itaanzisha soko moja kubwa la pamoja litakalohusisha nchi ishirini na sita.
Kukamilika kwa mpango huu huko Sharma Sheikh chini Misri itakuwa ni hatua ya awali tu, baada ya hapo mkataba huo utahitajika kuhakikiwa na bunge la kila nchi, kabla ya kuanza rasmi kufanya kazi.
Muungano kwa Afika si jambo jipya. Takribani nusu karne tangu Bara la Afrika lilipojipatia uhuru, serikali zimekuwa zikijadili namna ya kukuza biashara ya ndani.
No comments:
Post a Comment