Mwenyekiti wa Makampuni ya
Proin Group, Bw. Johnson Lukaza akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya iliyochezwa na washiriki wa
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mwaka 2014, uzinduzi huo
ulifanyika katika ukumbi wa sinema wa century uliopo Mlimani City,
Jijini Dar Es Salaam. Filamu hii ni moja ya filamu ambayo ina ubora wa
hali ya juu huku wadau waliofanikiwa kuitazama filamu hiyo kuvutiwa nayo
na kukubali kuwa ni filamu yenye viwango vya kimataifa na yenye
utofauti mkubwa na filamu nyingine za Kitanzania.

Bw. Lukaza akifurahia jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini, Mama Fisoo kabla ya uzinduzi wa
filamu ya Mpango Mbaya kuanza, uzinduzi huo ulifanyika jana katika
Ukumbi wa Sinema wa Century uliopo Mlimani city, Jijini Dar Es Salaam.

Muongozaji wa filamu ya Mpango Mbaya, Kalabani Kalabani akizungumzia juu ya filamu ya mpango mbaya aliyoiongoza.


Mmoja wa washiriki katika
filamu hiyo Anneth Peter (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mmoja
wa host wa TMT 2015 Mboto Haji (katikati) na Mwalimu wa washiriki wa
filamu Hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Mwl. Issa.

Mshiriki wa filamu ya Mpango
Mbaya Said (kulia) akijiachia mbele ya kamera ya Lukaza Blog kabla ya
uzinduzi wa filamu ya Mpango Mbaya uliofanyika Mlimani City.

Muongozaji wa Filamu ya Mpango
Mbaya, Kalabani Kalabani (katikati) akijadiliana jambo na mmoja wa
Washiriki wa filamu hiyo ambae ndie aliyekuwa mwigizaji msaidizi katika
filamu ya Mpango Mbaya Mzee Adolph.
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
No comments:
Post a Comment