Aliyekuwa makamu wa rais wa
shirikisho la soka duniani FIFA Jack Warner amesema katika hotuba ya
kushangaza aliyotoa katika runinga kwamba atafichua kila anachojua
kuhusu ufisadi katika shirikisho hilo.
Bwana Warner ambaye alisema
kuwa anahofia maisha yake pia amesema kuwa anaweza kuwahusisha maafisa
wa FIFA na uchaguzi mkuu katika taifa la Trinidad and Tobbago mwaka
2010.Ni mmoja wa watu 14 walioshtakiwa na Marekani kuhusiana na ufisadi katika FIFA. Mmoja wa maafisa wakuu wa FIFA na shahidi muhimu Chuck Blazer alikubali kuchukua hongo.
Afisa huyo alikiri kufanya hivyo mnamo mwaka 2013,ikiwa ni miongoni
mwa mashtaka yaliofunguliwa ambayo yameikabili FIFA na kumlazimu rais
wake Sepp Blatter Kujiuzulu.
Idara ya mahakama ya Marekani inadai
kuwa watu 14 walioshtakiwa walikubali hongo ya zaidi ya dola milioni 150
katika kipindi cha miaka 24.
No comments:
Post a Comment