Makao makuu ya jeshi la kulinda
usalama la Nigeria limehamisha kitovu cha operesheni ya kukabiliana na
wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram hadi mji wa Maiduguri.
Hatua
hii inafuatia ahadi ya rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alipokuwa
akiapishwa kuwa moja ya kauli mbiu ya utawala wake ni kukabiliana na
Boko Haram.
Msemaji wa jeshi kanali Sani Usman amesema kuwa wanajeshi wakuu wote wamehamia huko ilikuendesha operesheni dhidi ya kundi hilo.
Mji
huo ulioko kaskazini mwa taifa hilo tajiri zaidi barani Afrika kiuchumi
umekuwa kitovu cha mapigano makali baina ya wapiganaji wa Boko haram na
majeshi ya serikali.
Katika siku za hivi punde Maiduguri
Imeshuhudia visa vingi mno vya mashambulizi ya kujitolea mhanga ambayo
yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 80.
Rais mpya aliyechaguliwa
majuzi, Muhammadu Buhari, aliamuru kuhamishwa kwa kituo hicho hadi
Maiduguri kutoka mji mkuu wa Abuja - mahala ambapo aliapishiwa mwishoni
mwa mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment