Mguu huo wenye tofauti chache mno na ule halisi unahisi hata maumizi. Katika uvumbuzi huo wa Profesa Hubert Egger wa chuo kikuu cha Upper Austria, mguu huo bandia unatumia neva za mwili wa mtu aliyekatwa mguu wake.
Bwana Wolfgang Rangger alisema kuwa katika muda huo wa miezi sita anauwezo wa kubaini iwapo anakanyaga mawe, simiti,na hata nyasi.
''ninapo kanyaga jiwe,nahisi kitu kigumu na pia nikikanyaga mbao,pia najua kuwa kile nilichokanyaga ni tofauti.''
''Nimepata maisha mapya baada ya kupokea mguu bandia'' alisema Wolfgang Rangger.
No comments:
Post a Comment