Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
amesema kuwa, viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi
Duniani-G7, wamekubaliana kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinafaa kuendelea.
Bi Merkel amesema hadi pale muafaka wa kukomesha mapigano nchini Ukraine utakapoheshimiwa vikwazo sharti ziendelee.
Alishauri Ugiriki kuchukua hatua madhubuti ilikunusuru sarafu ya taifa hilo.
Viongozi hao wanafanya mazungumzo katika siku ya pili ya mkutano mkuu, wenye nia ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, huku pia swala la kuongezeka kwa makundi yenye itikadi kali likijadiliwa.
Bi Merkel pia amewataka wanachama wa G7 kuchangia hazina ya kuyasaidia mataifa maskini ambayo yanaathirika na mabadiliko ya hali ya anga.
Viongozi kutoka Nigeria na Tunisia watahudhuria kikao maalum, kuhusiana na hatari iletwayo na makundi yenye itikadi kali hasa yale ya Afrika.
Kwa mara ya pili tangu mzozo huo na Ukrain utokee rais Putin wa Urusi hakualikwa kwenye kikao hicho licha ya Urusi kuwa mwanachama wa G7.
No comments:
Post a Comment