Benki ya HSBC kupunguza matumizi yake
Mojawepo ya benki kubwa zaidi duniani ya HSBC imetangaza taratibu ya kutekeleza zoezi la kupunguza matumizi yake. Zoezi hilo litaiwezesha benki hiyo kuwasimamisha kazi zaidi ya wafanyikazi elfu ishirini kote duniani.
Benki
hiyo aidha itauza baadhi ya rasilimali zake nchini Brazil na Uturuki,
na kupunguza zaidi kiwango chake cha matumizi ya fedha kwa zaidi ya dola
bilioni mia tatu. Wengi wa wafanyikazi ambao watapoteza kazi watakuwa wale wa Uingereza, makao makuu ya sasa ya benki hiyo.
Uamuzi wa iwapo Benki hiyo itahamisha shughuli zake kutoka jijini London, utajulikana hatimaye mwaka huu.
Afisa
mkuu mtendaji wa benki ya HSBC, Stuart Gulliver, anasema kuwa muda
umewadia wa kutambua kuwa dunia imebadilika pakubwa, na kwamba ukuaji wa
uchumi barani Asia sasa ndio unaofaa kuangaziwa.
No comments:
Post a Comment