Serikali ya Hong Kong imetoa
tahadhari dhidi ya kusafiri kwenda nchini Korea Kusini, kufuatia kuwepo
mlipuko wa homa ya Middle East Respiratory Syndrome ambayo pia
inafahamika kama MERS nchini humo.
Onyo hilo linatolewa kwa safari ambazo si za lazima, ishara kuwa Hong Kong inaamini kwamba usafiri kwenda Korea kusini ni jambo ambalo ni hatari.
Wizara ya afya nchini Korea Kusini inasema kuwa watu 7 kwa sasa wameaga dunia kutokana ugonjwa huo. Kumeripotiwa visa 8 vipya vya homa ya MERS na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa kuwa 95.
No comments:
Post a Comment