Kocha wa Barcelona Luis Enrique amekataa kujadili hatma yake ama
kuthibitisha iwapo ataendelea kuifunza Barcelona licha ya kuipatia timu
hiyo mataji matatu.Enrique,katika msimu wake wa kwanza kama kocha
katika kilabu ya Barcelona baada ya kumrithi Gerardo Martino aliongeza
kombe la vilabu bingwa baada ya kupata lile la Copa Del Rey pamoja na La
liga kwa kuicharaza timu ya Juventus katika fainali iliochezwa katika
uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.
No comments:
Post a Comment