MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Malota Soma, amewataka viongozi
wa Simba kumaliza tofauti zao za kimkataba na winga Ramadhani Singano
‘Messi’ vinginevyo winga huyo akiondoka Simba haitapata mchezaji wa aina
hiyo kwa miaka 10 ijayo.
“Wachezaji wengi hawatofautiani, wengi wana staili
moja ya uchezaji, lakini Messi yupo tofauti kwani ana uwezo wa kipekee
wa kufunga mabao, anapiga chenga kali, anatengeneza nafasi za mabao,
anakaba bila ya kuogopa adui, lakini ni mchezaji mwenye nidhamu nzuri.
“Hivi mnafikiri kwa kizazi cha sasa mtapata wapi mchezaji wa aina hii?
“Nafikiri viongozi kama mmekosea, mwombeni radhi kisha mmalizane naye kwa manufaa ya Simba, bila hivyo shauri yenu.
“Nakumbuka mara ya mwisho kuona mchezaji wa aina
yake ni mwaka 1993 kwa Abdul Mashine aliyekuwa Simba na Thomas Kipese
Thomas walikuwa vizuri na hodari.”
No comments:
Post a Comment