Kilabu ya Manchester United inaamini
iko katika nafasi nzuri ya kumsajili Dani Alves kutoka Barcelona iwapo
kocha Louis Van Gaal anataka kumsajili beki huyo wa kulia.
Klabu ya PSG pia inamuania Alvez ijapokuwa kocha wake Laurent Blanc anaamini mchezaji huyo bado anataka kusalia Barcelona. Lakini maoni ya Old Trafford ni kwamba Alvez hangependelea kujiunga na PSG.
Mchezaji huyo wa Brazil anapokea kitita cha pauni 120,000 kwa wiki, fedha ambazo United inaweza kuzilipa bila kutoa jasho.
No comments:
Post a Comment