Pages

Sunday, 7 June 2015

Mawaziri wafanyiwa mabadiliko Sudan

Omar El Bashir
Rais wa Sudan Omar El Bashiri amewabadilisha mawaziri wake wa Ulinzi,mafuta na maswala ya kigeni katika mabadiliko makubwa tangu uchaguzi wa mwezi Aprili.

Sudan ikiwa imeathiriwa na ghasia za wenyewe kwa wenyewe na mgogoro wa kiuchumi,rais Bashir ameona umuhimu wa kufanya marekebisho,ijapokuwa raia wengi wa Sudan hawamuamini.

 
Kuondolewa kwa waziri wa Ulinzi Abdel Rahim Hussein ambaye ni mwandani wa rais huyo wa mda mrefu ni tukio ambalo halikutarajiwa.
Amepewa wadhfa wa chini kama Gavana wa jimbo la Khartoum. Rais Bashir na Hussein wanasakwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC kwa kutekeleza uhalifu katika eneo la Darfur.

No comments:

Post a Comment