 |
| Mwanamke aliyekuwa amezama akiokolewa. |
 |
| Kikosi cha waokoaji katika mto Yangtze wakiendelea na shughuli ya uokoaji. |
 |
| Kikosi cha uokoaji kikijiandaa kwenya kuwatafuta waliozama kwa ajali hiyo. |
 |
| Meli ya Dongfangzhixing iliyozama. |
 |
| Shughuli za uokoaji zikifanyika. |
 |
| Kikosi cha Uokoaji kikiwa kazini. |
 |
| Juhudi za uokoaji zikiendelea. |
 |
| Boti maalum za uokoaji. |
 |
| Waandishi wa habari wakichukua tukio hilo. |
 |
| Meli iliyozama. |
 |
| Mmoja wa wahanga wa ajali hiyo akifungwa kamba ili aokolewe kutoka majini. |
 |
| ...akiokolewa. |
 |
| Kikosi cha uokoaji cha dharula wakiendelea na oparesheni katika mto Yangtze. |
 |
| Wanakiji wa China wakitazama tukio hilo. |
 |
| Majeruhi katika ajali hiyo akipelekwa kwenye huduma. |
 |
| Ndugu wa baadhi ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo wakiwa na simanzi. |
 |
| Simanzi na majonzi zatawala. |
 |
| Waziri Mkuu wa China Li Keqiang (aliyeketi) akiwa kwenye Mkutano huko Beijing wakipanga mkakati na namna ambavyo uokoaji utafanyika. |
China
Meli ya Dongfangzhixing ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imepinduka na
kuzama jana usiku baada ya kukumbwa na dhoruba la upepo mkali katika
mto Yangtze kusini mwa China.
Taarifa zimeeleza kuwa, meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Mashariki
mwa Mji wa Nanjing kwenda Chongqing Kusini Magharibi mwa China ndipo
ilipozama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Meli hiyo ya Dongfangzhixing au Nyota ya Mashariki ilikuwa imewabeba
abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa Shirika la Usafiri na
wafanyakazi 47 wa meli hiyo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Serikali ya China, Xinhua ni
kwamba, kifaa maalum cha kurekodia video (CCTV Camera) kimeonesha watu
watano wakiwa mamefariki dunia kutokana na ajali hiyo na18 wakiwa
wameokolewa mpaka sasa. Kikosi cha Uokoaji kinaendelea na juhudi za
uokoaji kwa abiria wengine ambao hawajapatikana mpaka sasa. Japo kazi ya
uokoaji inakwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa zinazonyesha.
Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang amedfika eneo la tukio na kujionea maafa hayo.
Kwa upande wao Nahodha na Mhandisi Mkuu, ambao ni miongoni mwa
waliookolewa wamekaririwa wakisema kuwa, meli ilikumbwa na kimbunga
kikali ikapinduka na kuzama wakati huohuo.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo
inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha
shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.
Inasemekana kuwa, waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa
watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya
kitalii iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya Shanghai.
Ikumbukwe kuwa, mwezi Januari watu 22 walifariki dunia kwenye mto huo
wakati boti iliyokuwa kwenye majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang,
katika jimbo la Jiangsu.
NA BBC
No comments:
Post a Comment