| Mokhtar Belmokhtar |
Serikali ya Libya inayotambuliwa
kimataifa imesema mashambulio ya Marekani ya anga nchini Libya, yamemuua
mpiganaji mwandamizi wa Kiislam, Mokhtar Belmokhtar.
Mokhtar Belmokhtar mzaliwa wa Algeria anaamini kuamuru kufanyika kwa shambulio baya katika mtambo wa gesi nchini Algeria miaka miwili iliyopita ambapo wafanyakazi 38 wa mtambo huo waliuawa-- wengi wao wakiwa wageni waliuawa.
Kifo cha Belmokhtar kimekuwa kikiripotiwa mara nyingi katika siku zilizopita, lakini baadaye kubainika kuwa si habari za kweli.
No comments:
Post a Comment