Shirika linalopigania haki za
kibinadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vitendo vya vikosi vya
usalama nchini Kenya baada ya shambulizi la wanamgambo wa Al Shabaab
katika mkoa wa pwani vilichangia kuongezeka kwa taharuki nchini humo.
Human Rights Watch inayasema hayo kwenye ripoti iliyotolewa wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja tangu wanamgambo wa Al shabaab wauvamie mji wa Mpeketoni ulioko katika eneo la Lamu pwani ya kenya na kuwaua zaidi ya watu 60.
Wengi waliouawa walikuwa wanaume ambao hawakuwa waislamu.
No comments:
Post a Comment