KIUNGO wa zamani wa Yanga, Akida Makunda, amebainisha kuwa iwapo
kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’
angezingatia nidhamu ya juu, angekuwa kuwa mchezaji wa kipekee Simba
ambaye angeheshimika na kustaafu soka kama Steven Gerrard wa Liverpool.
| Aliyekuwa mchezaji wa Simba SC, Haruna Moshi "Boban" |
Makunda alisema: “Boban akiwa Simba alikuwa ni
mchezaji bora, aliheshimika sana lakini pia alikuwa ana jina kubwa, kitu
pekee kilichomtia doa ni ukosefu wa nidhamu ndani na nje ya uwanja.
“Naamini kama leo hii angezingatia nidhamu
angemalizia soka lake Simba na kuheshimika. Kwanza alikuwa ni mchezaji
ambaye alijitoa kwa Simba na hata hivyo naamini asingewahi kukubali
kusajiliwa timu kama Yanga kwasababu ya mapenzi aliyokuwa nayo kwa
Simba.
“Boban angeweza kubaki na kuwa kama baba wa timu,
nahodha na hata kiranja mkuu kwenye timu hiyo lakini alipoteza bahati
hiyo ambayo ingeweza kumpa sifa ya kihistoria kwenye soka la
Kitanzania.”
Mwaka 2013, Simba ilipokuwa ikinolewa na Kocha
Mfaransa Patrick Liewig, ilimsimamisha Boban na baadaye kuachana naye
kutokana na kosa la utovu wa nidhamu.
Baadaye alijiunga Coastal Union ambayo aliichezea
kwa msimu mmoja na kuachana nayo. Hivi sasa ni mchezaji wa Friends
Rangers ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
No comments:
Post a Comment