Willium Lucian 'Gallas'
|
KIRAKA Willium Lucian ‘Gallas’, amesema anaisikilizia timu yake
ya Simba kama itamwongezea mkataba mpya ama la, lakini kama dili hilo
litashindikana atatimkia katika timu nyingine za Ligi Kuu Bara kwani
zipo zilizoonyesha nia ya kumsajili.
Gallas ambaye ni zao la timu ya vijana ya Simba,
amemaliza mkataba klabuni hapo kama ilivyo kwa nyota wengine kadhaa
wakiwamo Ivo Mapunda, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu na Hassan Isihaka.
Kiraka huyo ambaye anamudu kucheza kama beki wa
kulia na kiungo mkabaji, alisema viongozi wa Simba wamemwambia asubiri
uamuzi wa benchi la ufundi kama wataendelea naye ama la.
“Mkataba wangu umemalizika, viongozi waliniambia
nisubiri na kama watakuwa hawanihitaji watanipa taarifa kwa njia ya
barua, kuna timu nyingine kwa sasa zimeonyesha nia ya kunipa usajili
lakini nasubiri kauli ya Simba kwanza,” alisema Galas.
Nyota huyo alisema amepanga kutumia kipindi hiki
cha mapumziko kufanya mazoezi ya gym na ufukweni ili kujiweka fiti zaidi
kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
“Nimepanga kufanya mazoezi ya gym na ufukweni,
angalau mara tatu kwa wiki ili nijiweke fiti zaidi, nataka kupandisha
kiwango changu, si unajua ligi ilivyo na ushindani?” alisema Gallas.
No comments:
Post a Comment