STRAIKA wa zamani wa Yanga, Idd Moshi ‘Mnyamwezi’, ametamka neno
ambalo halitafurahiwa na Mrisho Ngassa pamoja na mashabiki wake juu ya
kwenda kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini.
Mrisho Ngassa
|
Moshi, aliyewahi kutamba
pia na Milambo ya Tabora, alisema kuwa winga huyo wa zamani wa Yanga,
amechelewa mno kwenda kucheza Afrika Kusini kwani hatadumu muda mrefu
tofauti na kama angekwenda mapema.
Moshi alisema: “Ngassa angeweza kwenda Afrika
Kusini au Ulaya siku nyingi tu zilizopita, ingawa amepata nafasi lakini
hawezi kudumu kipindi kirefu kwani umri wake umeenda sana hivyo kwa
kifupi ni kama amechemsha kwa kiasi fulani.
“Tatizo letu sisi Watanzania huwa hatutaki
kujaribu vitu kipindi ambacho tunahitajika. Tunajaribu pale tu tunapoona
kuwa mambo yanaonekana kufika mwisho, hili lilitakiwa kuangaliwa mapema
na wachezaji kama Ngassa.
“Nafasi aliyoipata ni sehemu tu ya bahati yake
kisoka, hivyo anatakiwa acheze kwa nidhamu ya hali ya juu ili aweze
kufungulia milango wachezaji wengine wa Kitanzania kwenda kucheza Afrika
Kusini na nchi zingine.”
Ngassa ambaye tayari yupo Afrika Kusini,
amesajiliwa kwa mkataba wa miaka minne kuichezea Free State Stars
inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini baada ya kumaliza mkabata wake Yanga
hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment