Serena Williams amefanikiwa kutinga
fainali za michuano ya tenis ya French Open. Licha ya kujisikia kuumwa
Serena aliweza kupambana vikali na kumbwaga mpinzani wake Timea
Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu kucheza fainali za mwaka huu.
Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.
Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa.
Mapema katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii.
No comments:
Post a Comment