Sheria ya ndoa za jinsia moja yaanzishwa
Kinara mkuu wa chama cha upinzani
cha Labour nchini Australia, ameanzisha sheria inayokubalia ndoa ya
wapenzi wa jinsia moja, sheria ambayo inapingwa na Waziri mkuu wa nchi
hiyo, Tony Abbott.
Kiongozi huyo, Bill Shorten, amemtaka Bwana
Abbott kuwakubalia wanachama wa serikali wawe na uhuru wa kupiga kura
kuhusiana na swala hilo.
Abbot ambaye ni mfuasi wa kanisa katoliki
alikataa kura ya uhuru wa ndoa za jinsia moja na kusema kuwa lengo lake
kuu ni kuimarisha uchumi na usalama wa taifa.
No comments:
Post a Comment