Pages

Monday, 1 June 2015

STEPHEN WASSIRA ALIVYOTANGAZA NIA JIJINI MWANZA JANA

WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira jana ametangaza nia ya kuwania Urais akiwa jijini Mwanza. Mhe. Wassira alitangaza nia hiyo katika Ukumbi wa BOT uliopo jijini hapa na kuzungumza na mamia ya wanachama na watu mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais huku akitoa siri ya kuwafanya Watanzania kuwa na maisha mazuri pamoja na demokrasia inayozingatia usawa na haki kwa kila mtu katika nchi.

Nimeamua kuchukua uamuzi wa kutafuta ridhaa ya chama ambayo itaniwezesha kugombea katika nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu na kuahidi mambo mbalimbali ambayo atayafanya pindi atakapo pewa nafasi ya kuwa Rais.

Ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanaishi maisha ya amani na utulivu ili kuimarisha uchumi wa kila Mtanzania katika utawala bora na usimamizi mzuri wa raslimali za nchi.


Katika kuhakikisha nchi inabaki salama na watu wake wanakuwa na amani ya kuishi katika nchi yao ni kuimarisha sekta ya kilimo ambayo wananchi wengi waishio vijiji wanajishughulisha nayo kwa kuongeza fursa kwa wakulima kupatiwa vitendea kazi kama mbolea na matrekta ili kuondoa kilimo cha mkono ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya kilimo.

Aidha Wassira alieleza alivyojipanga kuwatafutia wakulima masoko ya kuuza bidhaa zao, kuimarisha miundo mbinu ya barabara kutoka vijijini, ujenzi wa reli pamoja na bandari ambazo zitasaidia kusafirisha bidhaa mbalimbali za kilimo kutoka maeneo tofauti ya nchi.

Vipaumbele vingine ambavyo aliviahinisha katika hotuba yake endapo akipewa ridhaa ya kuongoza nchi ataviimarisha ni pamoja na sekta ya uvuvi, mifugo, kuimarisha elimu, kufufu viwanda vya nafaka na nguo na kuongeza ajira kwa vijana kutokana na kutoa fursa nyingi za kiuchumi kwa vijana, kusimamia raslimali za nchi na kuhakikisha kila hospitali ya kijiji inapata dawa na huduma ya kutosha katika kuhudumia wananchi wa eneo husika na kupunguza adha ya mama wajawazito na wazee ambayo wanaipata kutokana na huduma kutokuwa nzuri.

Jambo lingine ambalo ameahidi kupambana nalo ni suala la rushwa kwa viongozi wa serikali kuhusika na upokeaji au utoaji wa rushwa akipatiwa ridhaa ya kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu ujao atahakikisha wale wote watakaohusishwa na ubadhirifu wa rasilimali za nchi wanachukuliwa hatua za kisheria kwa kufuata misingi ya utawala bora na haki kwa kila mwananchi au raia wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment