Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkaribisha Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Alvaro Rodriguez alipomtembelea kwa
ajili ya mazungumzo.
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez, alikutana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama na kufanya naye mazungumzo.
Miongoni mwa mambo waliyojadili ni maandalizi ya shughuli na matukio kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa mkoa alikubaliana na wazo hilo na kusema shughuli hiyo inafaa kufanyika katikati ya mwezi wa Agosti.
No comments:
Post a Comment