Saturday, 6 June 2015
Watu 400 wafariki katika mto Yangtse
Msemaji wa serikali nchini China
anasema kuwa karibu watu 400 wanahofiwa kuaga dunia wakati feri
ilipozama kwenye mto Yangtze siku ya jumatatu. Idadi hiyo imeongezeka kwa haraka baada ya makundi ya uokoaji kusaka vyumba vya feri hiyo.
Kwa sasa meli hiyo imendolewa majini kwa kutumia mitambo mikubwa. Jumla
ya watu 456 walikuwa ndani ya feri hiyo wakati ilipokumbwa na dhoruba
ambapo ni watu 14 tu walioripotiwa kuponea ajali hiyo. Ajali hiyo inaripotiwa kuwa mbaya zaidi nchini humo tangu miaka 60 iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment