MSAFARA wa Makongoro Nyerere ambaye ni
miongoni mwa wagombea urais, umepata ajali ya kupinduka kwa gari
wilayani Kasulu mkoani Kigoma leo.
| Gari lilivyopata ajali. |
Ajali hiyo imetokea wakati Makongoro na
msafara wake walipokuwa wakitoka mkoani Geita kuelekea Kigoma ikiwa ni
katika harakati za kusaka wadhamini wake watakaomuwezesha kujaza fomu
kuwania urais.
Taarifa zinasema kuwa, majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu kwa ajili ya matibabu.
| Wananchi wa Kasulu na Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio. |
Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya
simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Jafary Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema Jeshi la
Polisi Mkoani humo litatoa taarifa kamili baadaye, baada ya uchunguzi wa
awali kukamilika.
No comments:
Post a Comment