| Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiwakabidhi wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO mjini Mbeya vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa nyuki. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa kwa kupatiwa mizinga ya nyuki, mashine za kukamulia asali, vifaa vya kinga ya nyuki na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki. Wakishuhudia kutoka kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel mkoani Mbeya Saidi Zani |
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imewawezesha vijana wajasiriamali wa kikundi cha MINARACO kutoka mkoani
Mbeya wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki.
Kikundi hicho kinaundwa na vijana 76
walioamua kuungana na kujihusisha katika ufugaji wa nyuki ili kujikwamua
na changamoto za maisha. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho
kimewezeshwa kwa kupatiwa mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia
asali 1, vifaa vya kinga ya nyuki 2, chupa za lita 1, 400, chupa za
asali za lita 5, 200 na zana zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa
nyuki
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa
jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema, “vitendea kazi waliopatiwa ni
vyakisasa zaidi na vitasaidia kuboresha ufugaji huo na kuwawezesha
vijana hao kupata mavuno zaidi ya waliokuwa wakipata awali”.
Akiongezea amesema, “mpango huo wa
kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni sehemu ya mpango wa kampuni ya Airtel
wa kuwawezesha vijana ili kuboresha maisha yao na ya watu
wanaowazunguka”.
“Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona
ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana wenye umri kati
ya miaka 18-24 ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya
biashara kwa mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo”.
Wakipokea msaada huo wameishukuru, Airtel
kwa kujitoa kwa kuwasaidia vijana katika kutatua changamoto
zinazowakabili na kuahidi kutumia vifaa hivyo kwaajili ya kuongeza
uzalishaji ili kufikia malengo waliojiwekea katika kikundi hicho.
“Hatukuamini kuwa Airtel itakuja
kututembelea, kuangalia mahitaji yetu na hasa kwa kutupatia msaada wa
vifaa vya kisasa walivyo tupatia leo, tunawashukuru sana na tunaahidi
kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha tunakuza na kuendeleza ufugaji
bora wa nyuki” alisema mwakilishi wa kikundi hicho John Maige.
Akiongezea Maige alisema, “Awali tulikuwa
na changamoto ya uchache wa mizinga, vifungashio vya asali na soko la
uhakika, lakini Airtel imetusaidia kwa kutupa mafunzo na vifaa vya
kutosha vitakavyo tusaidia kupata Asali ya kutosha na yenye ubora mzuri
“.
Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi
nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na
kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana.
No comments:
Post a Comment